Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Thursday, 30 March 2017


MAELEKEZO YA ASKARI NA MAELEKEZO YA TAA AU ALAMA, NIFUATE YAPI?

SHERIA INASEMA HIVI: Anapokuwa amesimama trafiki barabarani kuongoza magari, alama nyingine zinaacha kutumika na malekezo ya huyo askari ndiyo yanayofuatwa.

Kwa hiyo ukikuta sehemu kuna alama ya 50kph ukapewa maelekezo ya kuongeza mwendo, unatakiwa kutii maelekezo hayo.

Ukikuta makutano yanayoongozwa na taa, taa nyekundu zikawaka askari akakuita upite, tii maelekezo hayo;
Ukifika sehemu haruhusiwi kugeuza (u-turn) askari akakuamuru kugeuza, fuata maelekezo ya askari;
Ukifika sehemu kuna zuio la kukunja kushoto ama kulia, askari aliyepo mbele yako akakuelekeza kukunja upande wowote ule, fuata maelekezo yake;
Ukifika sehemu hairuhusiwi kuegesha gari, askari akakuambia egesha hapa, tii maelekezo yake.
KWANI SHERIA INAMRUHUSU YEYE KUTOA MAELEKEZO HAYO kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) na (4) cha Sheria ya Usalama Barabarani.

RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE
ZA KITAIFA

Wednesday, 25 January 2017

MFAHAM MWANZILISHI WA PROGRAMM TUMISHI YA TusaliPamojaApp

Kwa majina  anaitwa Paulo C. Mushi Ni Mshiriki wa Kanisa La Wa Adventista Wa Sabato.,Na ndiye mmiliki na Mwanzilishaji wa Programm tumishi kwa simu za Android Inayoitwa TusaliPamojaApp.

Aliamua kuanzisha Programm hii ya Tusali Pamoja ili kuweza kusaidia wageni wawapo sehem ya ugenini kuweza kuliona kanisa la Wa Sabato kwa uharaka zaidi.Unaweza ku ipakua programm hiyo kwa kubonyeza hapa TusaliPamojaApp  .

Application hii aliiweka Play Store Mwaka jana  na kwa sasa anaendelea na Maboresho mengi ambayo yatapatikana katika toleo la Pili la Programm Hii tumishi kwa simu za Android.Ombi lake ni kuwezeshwa kupata taarifa za Makanisa mengi zaidi ikiwezekana yote Ya Wa Sabato Tanzania kwa haraka.

Yeye ni mzaliwa wa Kilimanjaro  ila amekulia Jijini Tanga,Ni Mtaalamu wa kuunda Programm tumishi za Simu Pamoja Na Tovuti lakini pia ni mtu aliye tayari kumuelekeza mwingine mwenye uhitaji wa kujua taaluma hii, na ndo mana aliamua kuanzisha group la Whatsapp kwa ajili ya vijana wa ki Sabato  ili kuwafundisha namna ya  kuunda prograam tumishi za simu pamoja na Tovuti. Kwa sasa ameanza na kuelekeza tovuti.
Ikiwa utahitaji kumpata basi waweza wasiliana naye kwa namba 0717331293.

Picha chini inamuonesha Akiwa na Mke wake Mpendwa Ambaye ni Mtumishi wa Kanisa ktika Conference ya S.E.C 

Friday, 23 December 2016

Tuesday, 20 December 2016

2G, 3G, 4G na 5G maana yake ni nini?


Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini?

G kwenye tarakimu hizi inawakilisha 'Generation', yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.
Hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.
Lakini wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.
Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.
Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.
Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu
Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa chini...




Kisha 2G ikaja na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi au arafa
Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi.
Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service).
Na pia simu za wakati huo zilikuwa na teknolojia ya GSM, GPRS, EDGE kama hizi zilizo hapa chini.

Kupiga simu kwa video kuliwezekana 2001

3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya smartphone zilianza kuuzwa madukani.
Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya. Angalau ilikuwa hatua fulani.
Na watu waliweza kupiga simu za video.



2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika
Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.
Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.

Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.
Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.




5G ndiyo mwendo kasi?
Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.
Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.
Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?



 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.