Jaji wa kiadventista msabato DAVID MARAGA aliye kataa kufanya kazi
katika siku ya Sabato(jumamosi),ameapishwa rasmi na kua jaji mkuu katika
nchi ya Kenya.
Katika ghafla ya kuapishwa kwake iliyofanyika katika ikulu ya Rasi wa
Kenya Uhuru Kenyatta,Jaji DAVID MARAGA alimualika Rais wa kanisa la
waadventista wa sabato Division ya Mashariki na kati Dr. BLASIOUS RUGURI
kwaajili ya kumuombea kabla hajaanza utekelezaji wa majukumu yake
mapya.
"Kama mkristo(mwadventista) niliadhimia kwamba kabla sijaanza mujukumu
yangu mapya kama jaji mkuu nitamshukuru Mungu kwa kunifikisha sehemu hii
ya Juu"Alisema Jaji mkuu David Maraga.
Dr.Blasious Ruguri alisema kua Jaji mkuu David Maraga ni mtu wa maombi na ni mfano wa kuigwa kwa waadventista wasabato wote.
Jaji mkuu David Maraga alisema kua itakua ni vigumu sana kwake kufanya
kazi katika siku ya sabato(Jumamosi) na kwamba atamuweka Mungu mbele ya
kazi yake.
Jaji mkuu David Maraga amechukua nafasi hiyo baada ya Aliye kua jaji mkuu kustaafu mwaka huu
Unknown
Author & Editor
Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.
0 comments:
Post a Comment