Katika sekta ya mawasiliano, ni
kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida
wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini?
Hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.
Lakini wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.
Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.
Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.
Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu
Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa chini...
2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika
Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.
Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.
Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.
Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.
5G ndiyo mwendo kasi?
Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.
Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.
Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?
0 comments:
Post a Comment