UBUNGO PLAZA -UKUMBI AMBAO MIKUTANO YA MAWASILIANO UNAOENDESHWA NA JIMBO LA KUSINI MASHARIKI MWA TANZANIA INAFANYIKA |
Kanisa la
waadventista wasabato jimbo la kusini mashariki mwa tanzania linaloundwa na
mikoa ya lindi, mtwara pwani pamoja na dar es salaam linakabiliwa na changamoto
za mila na desturi zac miongoni mwa wanajamii katika kufanikisha utume wa injili.
Hayo yameelezwa
na katibu wa jimbo la kusini mashariki mwa Tanzania mch. TOTO NDEGE BWIRE
KUSAGA wakati akizungumza na morning star radio katika ukumbi wa ubungo plaza
kwenye mkutano wa mawasiliano unaoendeshwa na jimbo la kusini la mashariki mwa
Tanzania.
Aidha Mch,Toto
amesema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa jimbo hilo bado swala la mila na
desturi limeendelea kuwa changamoto kwani wanakumbatia mila ambazo ni kinyume
na Imani ya kanisa la waadventista wasabato.
Pamoja na
hayo ameongeza kuwa mikoa ya mtwara na lindi inahitaji kupatiwa elimu ya
ujasiliamali ili kuondokana na umasikini unaotawala miongoni mwao.
Huu ni
mkutano wa Tatu na wa mwisho kuendeshwa na majimbo yaliyopo ndani ya Jimbo kuu
la Kusini mwa Tanzania ambapo mikutano kama hiyo imeendeshwa na Jimbo la
Mashariki kati mwa Tanzania na Jimbo la Nyanda za juu kusini.
0 comments:
Post a Comment