Mjue Mkurugenzi Mkuu Mpya TISS:
Jina kamili ni Dk Modestus Francis Kipilimba
Dini ni Mkristo.Ni mzaliwa wa Morogoro, Tanzania
Alifunga ndoa mwaka 1988, na ana watoto watatu. Kuanzia Januari mwaka 1973 hadi Novemba mwana 1976 amesoma Shule ya Sekondari Kingonsera iliyopo Mbinga mkoani Ruvuma. Kidato cha 5 na 6 amesoma Mkwawa High School iliyopo mkoani Iringa.
Shahada ya kwanza amesoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika masuala ya Kompyuta Shahada ya Uzamili (Masters Degree) alisoma nchini Uingereza katika chuo Salford, Manchester ambapo alisomea masuala la Kompyuta tangu Septemba 1992 hadi Novemba 1994.
Shahada ya Uzamivu (PhD) alisoma katika chuo hicho hicho cha Salford kilichopo Manchester Uingereza, kutoka Februari 2002 hadi Septemba 2005. Msomi huyo mwadilifu na mcha Mungu, akiwa nchini Uingereza amefundisha kwenye vyuo vikuu kadhaa nchini humo.
Dk.Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti Majanga (Director of Risk Management) Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuanzia mwaka 2011.Kabla ya kuwa Mkurugenzi wa idara hiyo alikuwa meneja wa Idara hiyo tangu mwaka 2009.
Tarehe 15 Februari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Kipilimba alijaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dickson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa. Tarehe 24 Agosti, 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.Mungu amjaalie kuitenda kazi yake vyema kwa faida ya taifa hili.
MUNGU AKUPE NGUVU, ULINZI NA UBUNIFU ZAIDI KATIKA KUFANIKISHA KILE ULICHOKABIDHIWA KUSIMAMIA.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 24 Agosti, 2016
amemuapisha Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Usalama wa Taifa.
Dkt. Modestus
Francis Kipilimba ameapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam na mara baada ya
kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa amekula kiapo cha
Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji
Salome Kaganda.
Kabla ya uteuzi
huo Dkt. Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus
Francis Kipilimba amechukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye
amestaafu.
Aidha,
Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika Makungu kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania Bara.
Kabla ya uteuzi
huo Bw. Robert Msalika Makungu alikuwa Afisa Ubalozi katika Ubalozi wa Tanzania
nchini Ethiopia.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na
nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.
Wakurugenzi na
Naibu Wakurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa waliopo wanaendelea na nafasi zao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU
Dar es Salaam
24 Agosti, 2016
0 comments:
Post a Comment