MAELEKEZO YA ASKARI NA MAELEKEZO YA TAA AU ALAMA, NIFUATE YAPI?
SHERIA INASEMA HIVI: Anapokuwa amesimama trafiki barabarani kuongoza magari, alama nyingine zinaacha kutumika na malekezo ya huyo askari ndiyo yanayofuatwa.
Kwa hiyo ukikuta sehemu kuna alama ya 50kph ukapewa maelekezo ya kuongeza mwendo, unatakiwa kutii maelekezo hayo.
Ukikuta makutano yanayoongozwa na taa, taa nyekundu zikawaka askari akakuita upite, tii maelekezo hayo;
Ukifika sehemu haruhusiwi kugeuza (u-turn) askari akakuamuru kugeuza, fuata maelekezo ya askari;
Ukifika sehemu kuna zuio la kukunja kushoto ama kulia, askari aliyepo mbele yako akakuelekeza kukunja upande wowote ule, fuata maelekezo yake;
Ukifika sehemu hairuhusiwi kuegesha gari, askari akakuambia egesha hapa, tii maelekezo yake.
KWANI SHERIA INAMRUHUSU YEYE KUTOA MAELEKEZO HAYO kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) na (4) cha Sheria ya Usalama Barabarani.
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE
0 comments:
Post a Comment