Tanzania ni miongoni mwa nchi kumi
za mwisho kwa viwango vya furaha kwa mujibu wa Ripoti ya Viwango vya
Furaha Duniani ya 2016 ambayo imetolewa leo.
Orodha hiyo
iliandaliwa kwa kuangazia pato la mtu kwa kila mwaka, miaka ambayo mtu
anatarajiwa kuishi, kuwa na mtu wa kutegemea kwa usaidizi, dhana ya
kuwepo uhuru wa kufanya maamuzi maishaji, uhuru kutoka kwa ufisadi, na
ukarimu miongoni mwa mengine.
Mataifa yaliyo kwenye kundi la
mataifa kumi ya mwisho ni Madagascar, Tanzania, Liberia, Guinea, Rwanda,
Benin, Afghanistan, Togo, Syria huku Burundi ikishika mkia.
Tanzania imo nambari 149 kati ya nchi 157 ikiwa na alama 3.695 kati ya alama 10 na Rwanda nambari 152 na alama 3.315.
Uganda
imo nambari 146 na alama 3.739, Malawi nambari 132 na alama 4.156,
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imo nambari 125 na alama 4.272 na Kenya
nambari 122 na alama 4.356.
Somalia imo nambari 76 na alama 5.44.
Ripoti
hiyo imetolewa mjini Roma, Italia huku ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha
Siku ya Furaha Duniani ya Umoja wa Mataifa tarehe 20 Machi.
Orodha hiyo imetayarishwa na shirika la maendeleo
endelevu ya Sustainable Development Solutions Network (SDSN) ambalo
lilianzishwa na Umoja wa Mataifa.
Denmark inaongoza kwa viwango vya furaha duniani ikiwa na alama 7.526 ikifuatwa kwa karibu na Uswizi, Iceland na Norway.
Finland, Canada, Uholanz, New Zealand, Australia na Sweden zinafunga kumi bora.
Marekani imo nambari 13 na Uingereza nambari 23.
Unknown
Author & Editor
Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.
0 comments:
Post a Comment