Picha
namba 12. Wakazi wa Chato wakifurahia Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa
Michezo wa Mazaina Wilayani Chato. PICHA
NA IKULU
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
|
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika
kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe
kuwa Rais, ambapo akizungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara uliofanyika
katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania
kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili
ambayo huambatana na masharti.
Dkt. Magufuli
amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na
kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na
utendaji kazi mahali pake pa kazi.
"Kwa hiyo ni
lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja
kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni
mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara
kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli,
Tanzania hii tutavuka" Amesema Rais
Magufuli.
Aidha, Rais
Magufuli amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu
serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma wanaolisababishia
taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la
"Kutumbua Majipu"
zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.
Dkt. Magufuli pia
amekumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu
Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa
mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi, kiongozi husika atakuwa
amedhihirisha kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.
Rais Magufuli amewapongeza
walimu kote nchini kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya changamoto ya
ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini
ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi
ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.
"Niziombe
kamati za shule zote Tanzania nzima, kama haziwezi kusimamia nidhamu ya
wanafunzi shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia kama wewe ni
Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka,
sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu Mkuu"
Alisisitiza Dkt. Magufuli.
Kuhusu tatizo la
wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni,
umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na
milioni 800, na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima
utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha
nyingi zaidi za watanzania.
Ametolea mfano wa
mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye alikuwa akilipwa
mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.
Pia Rais Magufuli
amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslai ya wafanyakazi kwa kupunguza
kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo,
lakini amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi
shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi
shilingi milioni 15.
Gerson Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Chato
29 Machi,
2016
0 comments:
Post a Comment