JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 15 Machi, 2016
amewaapisha wakuu wa mikoa 25, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA).
Walioapishwa na
Mikoa yao katika mabano ni Said Meck Sadiki (Kilimanjaro), Joel Nkaya Bendera
(Manyara), Dkt. Rehema Jonathan Nchimbi (Njombe), Said Thabit Mwambungu
(Ruvuma), Mhandisi Evarist Welle Ndikilo (Pwani), Magesa Stanslaus Mulongo
(Mara), Amina Juma Masenza (Iringa), John Vianney Kitayomba Mongella (Mwanza),
Halima Omary Dendegu (Mtwara), Daudi Felix Ntibenda (Arusha), Amos Gabriel
Makalla (Mbeya), Jordan Mugirage Rugimbana (Dodoma) na Aggrey Deaisile Joshua
Mwanri (Tabora).
Wengine ni Godfrey
Weston Zambi (Lindi), Kebwe Steven Kebwe (Morogoro), Anne Kilango Malecela
(Shinyanga), Anthony John Mtaka (Simiyu), Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Zelote Steven Zelote (Rukwa), Paul Christian
Makonda (Dar es salaam), Martine Reuben Shigela (Tanga), Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu (Kagera), Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya
Muhuga (Katavi), Meja Jenerali Emmanuel
Edward Maganga (Kigoma), Mhandisi Mathew John Mtigumwe (Singida).
Rais Magufuli pia
amewaapisha Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa hapa
nchini (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi
Valentino Longino Mlowola na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw.
Alphayo Japani Kidata.
Aidha, Mkuu wa
Mkoa wa Songwe Mteule Luteni Mstaafu
Chiku Galawa hakuapishwa leo kutokana na dharula ya kikazi, na tarehe ya kuapishwa kwake
itapangwa siku nyingine.
Mara baada ya
kukamilika kwa kiapo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ametoa ujumbe kwa Wakuu wote wa Mikoa, ambapo amewataka kwenda kufanya
kazi kwa kujiamini na kujielekeza kutatua kero za wananchi.
Maagizo mengine ya
Rais Magufuli ni pamoja na kuwataka wakuu hao wa mikoa kusimamia ulinzi na
usalama katika mikoa yao, na Kuhakikisha watu wanafanya kazi hususani vijana
ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
"Haiwezekani
Vijana wawe wanashinda vijiweni wanacheza pool, wakati wazee na akina mama wapo
mashambani wanalima. Kawahimizeni wafanye kazi, wasipofanya kwa hiari
walazimisheni kufanya kazi" Alisema Rais
Magufuli
Agizo jingine la
Dkt. Magufuli ni kuwataka kusimamia udhibiti wa fedha za umma katika
halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji na ametoa siku 15 kwa halmashauri
hizo pamoja na Wizara na Taasisi za Serikali kuondoa majina ya wafanyakazi hewa
katika orodha za mishahara ya watumishi wa umma.
Rais Magufuli pia
ametaka Wakuu wa Mikoa wakasimamie utekelezaji wa Elimu Bure ya kuanzia darasa
la kwanza hadi kidato cha nne, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha shule zina
madawati na majengo ya kutosha.
Dkt. Magufuli
amewasisitiza wakuu hao wa Mikoa kutosita kufanya maamuzi na kuchukua hatua
haraka, huku akitaka wawasimamie ipasavyo wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa
halmashauri, Makatibu Tarafa na Watendaji wa kata na Vijiji ili watekeleze
wajibu wao na waache kuwaonea wananchi wa chini.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
15 Machi,
2016
0 comments:
Post a Comment