Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Monday, 14 March 2016

Filled Under:

RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA TOTAL AFRIKA MASHARIKI JAVIER RIELO ALIYEAMBATANA NA UJUMBE WAKE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

ZA KITAIFA

Picha namba 1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Picha namba 2. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe walioambatana na  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Picha namba 3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo Ikulu jijini Dar es Salaam.


Picha namba 4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo

 

Picha namba 5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki,    Javier  Rielo  aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of ArmsKURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz              

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU,
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo  amemuhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha Mafuta kutoka nchini Uganda hadi bandari ya Tanga hapa Tanzania haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
Bw. Javier Rielo ametoa ahadi hiyo leo tarehe 14 Machi, 2016 alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es salaam.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi mapipa 200,000 kwa siku kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Katika Mazungumzo hayo Bw. Javier amemueleza Rais Magufuli kuwa Kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa.
Pamoja na kuukaribisha uwekezaji huo mkubwa kwa Tanzania, Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na ameshauri muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, amesema Wizara yake ipo tayari kuhakikisha mradi huo unafanikiwa, na itatoa ushirikiano wa kutosha kuharakisha utekelezaji wake.
Prof. Mhongo amebainisha kuwa licha ya kwamba hali ya kijiografia, hali ya hewa na bandari ya Tanga vinatoa mazingira bora ya kufanikiwa kwa mradi huo, Tanzania pia inatarajia kunufaika na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na ziwa Eyasi, ambazo zikikamilika kwa mafanikio inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
14 Machi, 2016

 


Unknown

Author & Editor

Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.