Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi( NACTE),Dr. Primus Nkwera amejiuzulu nafasi yake.
Uamuzi wa kujiuzulu kwa Dr. Nkwera ulitangazwa katika ofisi
kuu za Baraza hilo zilizopo Mikocheni Dar es Salaam na Mwenyekiti wa
Bodi,Mhandisi Steven Mlote na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kuangua
kilio.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha wafanyakazi wote
wa baraza hilo,Mlote alisema Dr. Nkwera amejiuzulu ili kulinda hadhi ya
Nacte kutokana na habari iliyoandikwa na Gazeti la Dira ikimtuhumu mambo
mbalimbali.
Gazeti hilo la Dira la Jumatatu tarehe 07/03/2016 toleo
no.405 lilimtuhumu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dr.Primus Nkwera kughushi
vyeti vya shahada ya uzamivu baada ya kusomeshwa na serikaliAfrika
Kusini na kufeli.
Mlote alisema kwa mujibu wa Dr. Nkwera, nafasi hiyo
haipaswi kushikwa na mtu mwenye tuhuma ya aina yoyote, na ametafakari na
kuona ajiweke kando na uongozi wa Nacte ili uchunguzi ufanyike akiwa
pembeni.
"Tumetumia muda mwingi kutafakari hoja ya Dr. Nkwera na
hatimaye tumekubali kujiuzulu kwake kwa shingo upande," alisema Mlote na
kuongeza:
"Kazi kubwa iliyofanywa na Dr. Nkwera akiwa kiongozi wa
Nacte inafahamika na kila mmoja, vilio na machozi ya wafanyakazi wenzake
yanadhihirisha kuwa kujiuzulu kwake kunaacha simanzi kubwa.
"Najua mmepata mshtuko mkubwa, lakini Dr Nkwera hajafa,
yuko hai na huyu bado ni mtumishi wa serikali. Alichofanya ni kuamua
kuachana na ukatibu utendaji.
"Tutaendelea kumtumia itakapobidi kwa ushauri.Wakati
mwingine lazima mkubaliane na hali hii, lakini pia endeleen kuchapakazi
kwa ufanisi kama kawaida kana kwamba bado mko na Dr. Nkwera."
Kutokana na kujiuzulu kwake, Mlote alisema bodi imemteua
Mkurugenzi wa Mitaala wa Nacte, Dr Adolf Rutayunga kukaimu nafasi hiyo
wakati taratibu nyingine zikiendelea.
Akizungumza na wafanyakazi hao, Dr. Rutayunga alisema viatu
alivyoviacha Dr. Nkwera ni vikubwa kwake, lakini akaahidi kuendeleza
yote aliyoyaacha.
|
0 comments:
Post a Comment