|
Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imepokea msaada wa fedha kiasi
cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kwaajili ya kusupport mamlaka ya mapato katika
kuongeza kipato nchini na kuongeza nguvu katika kuzuia mianya ya ukwepaji
kodi kwa Watanzania.
Akizungumza
mbele ya waandishi wa habari, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji amesema Serikali ya Kifalme ya Norway imetoa msaada kwa
Tanzania katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha kwamba tunaweza
kuzuia wanaokwepa kulipa kodi‘
Dkt ameeleza kuwa Wizara ya fedha inataka kuondoka kutoka katika bajeti
ya utegemezi na kwenda katika bajeti ya kujitegemea, lakini haiwezi kufika huko
bila kuimarisha ukusanyaji wa mapato
Kwahiyo tunaishukuru sana Serikali ya Norway kwa
msaada huu na pia tunawaahidi tutazitumia vizuri katika kuimarisha mamlaka yetu
ya mapato na kazi zake kwa ujumla.
|
Unknown
Author & Editor
Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.
0 comments:
Post a Comment