RUKWA
Serikali mkoani Rukwa imeanza kuweka mikakati ya kujenga
hospitali ya kisasa ya Rufaa ili kukabiliana na changamoto ya msongamano mkubwa
wa wagonjwa wanaolazwa kwenye hospitali ya mkoa huo kinyume na uwezo wake.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mkuu wa wilaya
Sumbawanga Dk. Halfan Haule amesema licha ya idadi kubwa ya wagonjwa lakini pia
hospitali hiyo ya Rufaa mkoa wa Rukwa inakabiliwa na changamoto nyingi za
kitaalamu sanjari na vifaa Tiba hivyo kutoa wito kwa wadau kushirikiana na
serikali kuhakikisha wanasaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali hospitalini
hapo.
Kufuatia hali hiyo Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia kwa Meneja
wa Mfuko huo wa Taifa Bw.Amin Laban umetoa msaada wa mashuka Hamsini zenye
thamani ya takribani Milioni mbili ili kuweza kusaidia wagonjwa wanaolazwa huku
wakiahidi kuendelea kusaidia kila watakapopata fursa ya kibajeti.
Halmashauri zote za mkoa wa Rukwa kwa muda mrefu zimekua
zikisuasua katika utoaji wa huduma za afya kutokana kukosa hospitali za
wilaya ambapo Halmashauri ya wilaya Nkasi imekuwa ikitegemea hospitali ya NDDH
ya Namanyere, sawa na wenzao wa Manispaa ya Sumbawanga ambao nao hutegemea
hospitali ya Dr. Atman, ambazo ni mali ya kanisa Katoliki.
Wakati wenzao wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo wao hutumia
kituo cha Afya cha Matai kama hospitali ya wilaya na Halmashauri ya Sumbawanga
hutegemea kituo cha Afya cha Laela.
0 comments:
Post a Comment