Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Julai, 2016
amemteua Bw. Deogratius John Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani
Dodoma.
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi amesema Bw. Deogratius John Ndejembi anachukua
nafasi iliyoachwa na aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. John Ernest
Palingo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho wa Bw.
John Ernest Palingo kwenda Wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Mhe. Rais
Magufuli kuridhia maombi ya Bw. Ally Masoud Maswanya aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.
Bw. Deogratius
John Ndejembi atakula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma siku ya
Jumanne tarehe 12 Julai, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment