Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Thursday 30 June 2016

Filled Under:

MCHUNGAJI MWASOMOLA APATA AJALI

MAKANISANI



Mwenyekiti wa Conference ya Nyanda za Juu Kusini ya kanisa la waadventista wasabato Mchungaji Kenan Mwasomola Amepata Ajali Jana majira ya Saa 2 Usiku eneo la Nyandekwa Katikati ya Igunga na Nzega Wakati Akielekea Kirumba jijin Mwanza kwa Sherehe ya Jubilee ya miaka 50 akiwa na Gari la Office.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Shuhuda wa Ajali hiyo Ambaye pia alikuwa ndani ya Gari hilo Mch. Bambaganya Amesema Mchungaji Ameumia Maeneo ya Mbavu na Mke wa Mchungaji Mwasomola  Ameumia Shingoni na Begani na Tayari wote wamelazwa  Hospitali ya Mission ya Nkinga Na hali zao Zinaendelea Vizuri.
Mchungaji Bambaganya ameeleza kuwa Sababu ya Ajali ni Tuta lililo kuwa katika barabara ambayo lami imekwanguliwa na hakuna alama yeyote ya kuelekeza. Jambo lililo sababisha Gari kubilingita juu chini na hatimaye kusimama.
Kwa Mujibu wa wenyeji wa eneo hilo wameiambia Morning star Radio kuwa  Tuta hilo limesha sababisha Ajali nyingi zilizo poteza maisha ya watu.

Unknown

Author & Editor

Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.