TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Hamphrey Polepole
kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkoani Mara.
Bw. Hamphrey Polepole
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Musoma,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (Mstaafu) Zelothe Steven ambaye sasa ni
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
Uteuzi wa Bw.
Hamphrey Polepole umeanza leo tarehe 18 Aprili, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
18 Aprili,
2016
0 comments:
Post a Comment