Katibu wa Baraza la Elimu nchini
Kenya,Fred Matiangi ameonya kuwa serikali haitaruhusu kuona taasisi za
Elimu zikiwalazimisha Wanafunzi wa Kiadventista kwenda shule siku ya sabato
nchini humo kwani ni kinyume cha mafundisho ya Kanisa la Waadventista Wa
Sabato.
Matiangi amesema wanafunzi wa
kiadventista nchini humo wanapaswa kupewa kipaumbele na kuwataka viongozi wa
taasisi za elimu nchini humo kutotoa mafunzo ya ziada siku ya sabato ili
kutowanyima wanafunzi wa kiadventista haki yao ya kuabudu,huku akisisitiza kuwa
serikali ya Kenya itahakikisha jambo hilo halifanyiki.
Pia ametoa tahadhari kwa walimu wa
taasisi za elimu kutowaruhusu wahubiri wanaotembelea taasisi hizo
kwa kuwa wana ajenda zao binafsi.
Matiangi amesema utafiti umebaini
kuwa baadhi ya wahubiri wamekuwa wakiwashawishi wanafunzi kujiunga na taasisi
ambazo hazijasajiliwa na zenye ajenda binafsi zisizojulikana.
Asilimi 82.6 ya idadi ya watu
nchini Kenya ni waumini wa Madhehebu ya Kikristo huku Uislamu ukishika nafasi
ya pili kwa kuwa na asilimia 11.1 ya idaidi ya Watu,wengine ni Wabudha,Wahindu
na Imani ya Asili huku kukiwa na Waadventista Wasabato wanaokadiliwa kuwa
600,000 nchini humo.
HAPA KAAZI TU.....MAGUFULI WA HUKU...JE TANZANIA MWAFATA MKONDO HUU AMA PIA MWAWALAZIMISHA WANAFUNZI WA ADVENTISTE KUFIKA SHULENI SIKU YA SABATO??
ReplyDelete