UNCLE PRINCE,RAFIKI WA WOTE

Kaa karibu yangu upate kujua habari za Wanakwaya & Na kwaya zetu, enjoy!

Featured Coupons

Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Latest Coupons

Tuesday, 20 June 2017

ITAZAME TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA MH MRISHO M. GAMBO


ZA KITAIFA

Wednesday, 5 April 2017

HOSPITALI YA KISASA YA RUFAA INATARAJIWA KUJENGWA MKONI RUKWA



RUKWA                                                    
Serikali mkoani Rukwa imeanza kuweka mikakati ya kujenga hospitali ya kisasa ya Rufaa ili kukabiliana na changamoto ya msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaolazwa kwenye hospitali ya mkoa huo kinyume na uwezo wake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mkuu wa wilaya Sumbawanga Dk. Halfan Haule amesema licha ya idadi kubwa ya wagonjwa lakini pia hospitali hiyo ya Rufaa mkoa wa Rukwa inakabiliwa na changamoto nyingi za kitaalamu sanjari na vifaa Tiba hivyo kutoa wito kwa wadau kushirikiana na serikali kuhakikisha wanasaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali hospitalini hapo.

Kufuatia hali hiyo Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia kwa Meneja wa Mfuko huo wa Taifa Bw.Amin Laban umetoa msaada wa mashuka Hamsini zenye thamani ya takribani Milioni mbili ili kuweza kusaidia wagonjwa wanaolazwa huku wakiahidi kuendelea kusaidia kila watakapopata fursa ya  kibajeti.

Halmashauri zote za mkoa wa Rukwa kwa muda mrefu zimekua zikisuasua katika utoaji wa huduma za afya  kutokana kukosa hospitali za wilaya ambapo Halmashauri ya wilaya Nkasi imekuwa ikitegemea hospitali ya NDDH ya Namanyere, sawa na wenzao wa Manispaa ya Sumbawanga ambao nao hutegemea hospitali ya Dr. Atman, ambazo ni mali ya kanisa Katoliki.

Wakati wenzao wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo wao hutumia kituo cha Afya cha Matai kama hospitali ya wilaya na Halmashauri ya Sumbawanga hutegemea kituo cha Afya cha Laela.
ZA KITAIFA

KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO JIMBO LA KUSINI MASHARIKI MWA LINAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA MILA NA DESTURI ZA MIONGONI MWA WANAJAMII KATIKA KUFANIKISHA UTUME WA INJILI.

UBUNGO PLAZA -UKUMBI AMBAO MIKUTANO YA MAWASILIANO UNAOENDESHWA NA JIMBO LA KUSINI MASHARIKI MWA TANZANIA INAFANYIKA           



Kanisa la waadventista wasabato jimbo la kusini mashariki mwa tanzania linaloundwa na mikoa ya lindi, mtwara pwani pamoja na dar es salaam linakabiliwa na changamoto za mila na desturi zac miongoni mwa wanajamii katika kufanikisha utume wa injili.

Hayo yameelezwa na katibu wa jimbo la kusini mashariki mwa Tanzania mch. TOTO NDEGE BWIRE KUSAGA wakati akizungumza na morning star radio katika ukumbi wa ubungo plaza kwenye mkutano wa mawasiliano unaoendeshwa na jimbo la kusini la mashariki mwa Tanzania.

Aidha Mch,Toto amesema kuwa pamoja na juhudi zinazofanywa jimbo hilo bado swala la mila na desturi limeendelea kuwa changamoto kwani wanakumbatia mila ambazo ni kinyume na Imani ya kanisa la waadventista wasabato.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa mikoa ya mtwara na lindi inahitaji kupatiwa elimu ya ujasiliamali ili kuondokana na umasikini unaotawala miongoni mwao.

Huu ni mkutano wa Tatu na wa mwisho kuendeshwa na majimbo yaliyopo ndani ya Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania ambapo mikutano kama hiyo imeendeshwa na Jimbo la Mashariki kati mwa Tanzania na Jimbo la Nyanda za juu kusini.
MAKANISANI ZA KITAIFA

Thursday, 30 March 2017


JE UNAFAHAMU MADHUMUNI YA USAJILI WA VYOMBO VYA MOTO?

Kwa watu wengi, uelewa wao juu ya madhumuni ya usajili wa vyombo vya moto unaishia kwenye kukusanya mapato. Ukweli ni kwamba, pamoja na hilo kuwa ni moja kati ya madhumuni ya usajili wa vyombo vya moto, bado kuna madhumuni mengine mengi ya usajili wa vyombo vya moto kama vile; kuonesha uhalali wa umiliki wa chombo husika, ndio maana kadi ya umiliki wa chombo husika hutolewa baada ya usajili.

Lakini pia usajili wa vyombo vya moto una dhumuni la kuonesha matumizi ya chombo kilichosajiliwa kwa maana kwamba kama chombo kimesajiliwa kwa matumizi *binafsi* ama kwa matumizi ya *biashara.* Zaidi ya hayo usajili wa vyombo vya moto unadhumuni la kuonesha aina ya chombo, kama ni gari na ni gari la aina gani, ama ni pikipiki, trela, trekta mtambo, nakadhalika.

Dhumuni jingine la usajili wa vyombo vya moto ni kurahisisha uchunguzi wa uhalifu endapo utafanywa kuhusisha chombo cha moto. Lakini pia usajili wa vyombo vya moto hurahisisha utoaji wa taarifa mbalimbali zinazohusu vyombo vya moto kwa taasisi nyingine. (Information/Statistical data), mfano ajali za kugonga na kukimbia (Hit & Run accidents).


Ndio maana Kifungu cha 8 (i) cha Sheria ya Usalama barabarani namba 30/1973 (CAP 168 RE.2002) inaeleza kuwa hairuhusiwi kwa mtu yeyote *kuendesha chombo cha moto ambacho hakijasajiliwa.


Kipengele (2) cha sura hiyo hiyo kinaeleza adhabu kwa mtu atakayekamatwa akitumia chombo cha moto ambacho hakijasajiliwa kuwa ni pamoja na faini isiyozidi elfu hamsini za kitanzania au kifungo kisichozidi miaka mitano.

ANGALIZO HAPA NI KWAMBA , kumekuwa na taarifa za mitaani kuwa unaruhusiwa kutumia chombo cha moto kisichosajiliwa mpaka saa 12 jioni na siku za mwisho wa wiki na sikukuu. Taarifa hizo sio sahihi, sheria inasema kwamba *hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutumia chombo cha moto ambacho hakijasajiliwa.
Hapa juu nimetaja sheria ya usalama barabarani, Sheria ya Usalama Barabarani namba 30/1973 (CAP 168 RE.2002). Lakini si sheria hiyo pekee inayosimamia usajili wa vyombo vya moto.

Kuna sheria nyingine kama vile, Sheria ya Usajili na Ubadilishaji wa Umiliki wa gari ya mwaka 1972. (Motor Vehicles Tax on Registration and Transfer Act of 1972). Hivyo kununua chombo cha moto chenye usajili wa mtu mwingine na kukitumia bila kubadilisha umiliki ni kosa kisheria. Hata hivyo kosa hili linaonekana ni la kawaida sana kwa jamii hasa kutokana na ugumu wa maisha na watu wengi kushindwa kununua magari mapya na hivyo kulazimisha kununua magari mikononi mwa watu wengine yakiwa tayari yalisajiliwa kwa matumizi yao.

Sheria inamtaka kila mmoja kubadili umiliki mara baada ya kununua.
Pia kuna kanuni mbalimbali za usalama barabarani zilizoundwa chini ya sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002. Moja wapo ikiwa ni Road Traffic Motor Vehicle Registration 2001). Sheria zote hizi zina lenga kuhakikisha kuwa kila mmoja anafuata taratibu sahihi za matumizi ya vyombo vya moto.

RSA TANZANIA

 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.