Picha namba 4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John
Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la
Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA
IKULU
Mwenyekiti wa
Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Alhamisi ya tarehe 08
Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa
Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.
Baaada ya
mazungumzo hayo,Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca
Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania
kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya afrika ya
Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.
"Tumefarijika
kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt Magufuli kama
Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana na viongozi wenzake
wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudani ya
Kusini liwe Taifa lenye amani,hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi
yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio
chetu"
Rais Magufuli kwa
upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia
muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko
yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.
"Mama Rebecca
hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudani ya
Kusini hivyo,ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa
amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudani ya Kusini"
|
0 comments:
Post a Comment