Rais mteule wa Marekani Donald Trump amewasili katika Ikulu ya White House, kwa mujibu wa maafisa nchini Marekani.
Anatarajiwa kuwa kwenye mazungumzo na Rais Obama wakati huu.
Licha ya tofauti zao, bwana Obama siku ya Jumatano alikishauri kikosi chake kufanya jitihada zaidi kuhakisha kuwa kuna mafanikio kwenye shughuli ya kupokeza madaraka kwa Republican mwezi Januari.
Mapema kikosi cha kampeni ya Trump kilikutana na washauri kujadili masuala kuhusu siku za kwanza 100 za Trump kama rais na uteuzi muhimu katika nyadhifa za serikali.
Majina yaliyotajwa ni kati ya wale waliomuunga mkono Trump kutoka mwanzo akiwemo aliyekuwa spika Newt Gingrich, maseneta Jeff Sessions na Bob Corker pamoja na aliyekuwa meya wa New York Rudy Giuliani.
0 comments:
Post a Comment