Rais mteule wa Marekani Donald Trump
amesema kuwa ni ''heshima'' kubwa kukutana na rais Barrack Obama katika
mazungumzo ya mpito yaliofanyika katika ikulu ya White House.
Bwana Obama amesema kuwa ametiwa moyo kuhusu mazungumzo yao ya maswala mbalimbali yaliochukua zaidi ya saa moja.Bwana Trump ametilia shaka uraia wa rais Obama na kuapa kuharibu ufanisi wake wakati wa utawala wake.
Wakati wa kampeni bwana Obama alisema kuwa bwana Trump 'hafai' kuongoza Marekani.
Hatahivyo Obama alisema kuwa ''anamuunga'' mkono baada ya kumshinda Hillary Clinton.
Baada ya mkutano huo wa ikulu rais Obama alisema kuwa kipaombele chake sasa katika miezi miwili ijayo ni kuhakikisha kuwa kundi litakalosimamia shughuli za mpito linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wamezungumza sera za nyumbani pamoja na zile za kigeni na kwamba amefurahishwa na maoni ya Donald Trump kwamba yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika maswala yanayokabili Marekani.
Bwana Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na rais Obama katika siku zijazo.
0 comments:
Post a Comment