Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexender Pastory Mnyeti ameamuru kukamatwa
kwa Diwani wa kata ya Lemanyata Losyeku Kilusu mkoani Arusha, wenyeviti
wa vitongoji saba, wenyeviti wa vijiji watatu kwa thuma za kujihusisha
na kilimo cha bangi pamoja kuuza. Mnyeti amemtaka diwani wa kata hiyo
ajisalimishe polisi kutokana na kata yake kukutwa na Hekari zaidi ya
nane za bangi.
DC Mnyeti amesema, ''‘wenyeviti wa kitongoji,
watendaji wa vijiji hii ni biashara yao namba moja haiwezekani mashamba
ya bangi yanalimwa, watu wanalima mnaona, mpaka yanafikia kimo hiki
mnaona, mpaka mimi mkuu wa wilaya nakuja mpaka huku nyinyi pengine hamna
taarifa za hiki kilimo''
''OCD nakuagiza kamata watu hawa wote,
weka ndani mpaka wakuambie nani analima hii bangi, maana kwanza hawako
tayari hata kusema, halafu hili zao sitaki kuliona msikate kwa chini
mng’oe kabisa,'' amesema DC Mnyeti.
Tuesday, 18 October 2016
Filled Under:
MKUU WA WILAYA YA ARUMERU ATOA AMRI YA KUKAMATWA DIWANI NA WENYEVITI WA VIJIJI
By
Unknown
Dated
07:39
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment