Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe
Magufuli, ameiomba wizara ya ujenzi kubadilisha jina la Daraja la kigamboni na
kuliita daraja hilo Daraja La Nyerere ili kumuenzi baba wa Taifa aliyekuwa na
ndoto ya kujenga daraja hilo kabla ya uhuru wa Tanzania.
Rais
ameyasema hayo wakati akizindua daraja hilo mchana wa leo katika eneo la
kigamboni jijini Dar es salaam, ambapo Rais amewapongeza viongozi waliopita
katika awamu ya nne kwa namna walivyoanzisha ujenzi wa daraja hilo wakati yeye
akiwa waziri wa Ujenzi.
Wakati zoezi
hilo likiendelea Rais amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe kufuatia shutuma za
matumizi mabaya ya madaraka zilizoelekezwa kwake na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda aliyesema hawezi kufanya nae kazi.
Kabwe akiwa
Mkurugenzi Mkuu wa Jiji la Dar es Salaam anashutumiwa amehusika kwa kuiongezea
kampuni ya utozaji ushuru wa parking jijini Dar es Salaam, pamoja na ongezeko
la kiwango cha faini halali ya shs 20,000/=hadi shs 80,000/=kwa kila kosa la
kuegesha gari vibaya, kuongeza muda wa mkataba kinyemela pamoja na tozo kwa kila mtu aingiapo katika kituo cha
mabasi cha Ubungo ya sh 200/=isiyoeleweka inakopelekwa.
Daraja la
kigamboni ambalo kwa sasa litaitwa daraja la Nyerere lina urefu wa mita 680 na
barabara unganishi upande wa Kurasini na
Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5 limeanza kujengwa mwaka 2012 na hii leo
limezinduliwa rasmi na Rais kwa ajaili ya matumizi kwa wananchi, ambapo Rais
ameeleza kuwa serikali imetoa asilimia 40 na asilimia 60 za gharama zimetolewa
na shirika la hifadhi ya jamii NSSF.
0 comments:
Post a Comment