Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Jim James Yonazi
kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Rais
Magufuli amefanya uteuzi huo kuanzia tarehe 18 Juni, 2016.
Kabla ya uteuzi
huo Dkt. Jim James Yonazi alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa katika Tume
ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Dkt. Jim James
Yonazi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Gabriel Nderumaki ambaye uteuzi
wake ulitenguliwa.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam
21 Juni,
2016
0 comments:
Post a Comment