 |
Visa vya usafirishaji wa bidhaa
zilizopigwa marufuku kama vile zile zilizotengenezwa kutokana na Pembe
na Ngozi ya wanyama wa Pori pamoja na mihadarati vimekuwa vikikithiri
kutokana na kutokuwepo kwa mbwa maalum wa kunusa na kukagua bidhaa
zinaposafirishwa kupitia viwanja vya ndege au Bandari.
Tanzania ni
mojawapo ya mataifa yalioathirika kutokana na usafirishaji wa bidhaa
aina hizo kinyemela. Hata hivyo hali hii huenda ikakoma kwani Serikali
ya Tanzania sasa imepokea mbwa maalum wa kuwasaidia maafisa wa usalama
na wakaguzi katika operesheni za kunasa bidhaa zilizopigwa marufuku.
Serikali
ya Marekani kupitia Ubalozi wake wa Dar es Salaam, imetoa msaada wa
Mbwa wanne na Mafunzo yaliyofanyika katika Chuo cha Forodha na Ulinzi wa
Mipaka ya Marekani (CBP).
Mbwa hao watasaidia Usalama katika
Viwanja vya Ndege na Bandari kwa kubaini bidhaa haramu zinazovushwa
katika maeneo kama hayo zikiwamo nyara za serikali na madawa ya kulevya.
Askari
wanne watanzania wanaowasimamia mbwa hao wanatoka katika katika Kikosi
cha Mbwa na Farasi na wamepata mafunzo na kufuzu katika chuo kilichoko
El Paso, Texas Marekani.
“Ni msaada ambao umekuja wakati mzuri,
ambapo wanyama pori maisha yao yako hatarini kuliko wakati wowote huko
nyuma.” Alisema Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Profesa
Jumanne Maghembe.
Bi Virginia Blaser Balozi Msaidizi wa Ubalozi wa
Marekani alisema watu wanaojihusisha na Biashara haramu hawajali juu ya
Tanzania na Watu wake bali wanajali Pesa tu ndiyo maana Marekani
imeamua kusaidia kupambana na hali hiyo ili watu hao wakumbane na mkono
wa Sheria.
|
Unknown
Author & Editor
Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.
0 comments:
Post a Comment