Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Makenya Abraham
Honoratus Maboko kuwa Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 23 Juni, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
inasema uteuzi huu umeanza tarehe 21 Juni, 2016.
Prof. Makenya
Abraham Honoratus Maboko anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Cuthbert Mhilu
ambaye amemaliza muda wake.
Prof. Maboko ni
Mhadhiri wa Jiolojia katika Chuo Kikuu
cha Dar es salaam (UDSM).
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Omari Ali Amir kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Uvuvi wa Bahari Kuu.
Kabla ya uteuzi
huo Dkt. Omari Ali Amir alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Taarifa ya Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi inasema uteuzi wa Dkt. Omari Ali Amir umeanza
tarehe 21 Juni, 2016.
Utaratibu wa
kujaza nafasi ya Mkurugenzi Mkuu na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi
wa bahari kuu ni wa kubadilishana kila baada ya miaka mitatu kati ya Tanzania
Bara na Tanzania Zanzibar, ambapo Mkurugenzi Mkuu akitoka upande mmoja wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania basi Naibu Mkurugenzi Mkuu hutoka upande
mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinyume chake.
0 comments:
Post a Comment