Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Monday, 23 May 2016

Filled Under:

RAIS MAGUFULI ATEUA NAIBU MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NA MSHAURI WAKE WA UCHUMI

ZA KITAIFA
Profesa Longinus Rutasitara




Picha. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng.  John Kijazi akisoma taarifa ya Uteuzi wa viongozi mbalimbali uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gerson J. Mdemu kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Gerson J. Mdemu alikuwa Karani wa Baraza la Mawaziri (Cabinet Clerk).
Bw. Mdemu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Tulia Ackson ambaye amechuguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Mshauri wa Rais, masuala ya uchumi.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Longinus Rutasitara alikuwa Mhadhiri wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi leo tarehe 23 Mei, 2016 imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.


Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
23 Mei, 2016
 






Unknown

Author & Editor

Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.