Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Wednesday, 20 April 2016

Filled Under:

TANAPA KUFANYA USAFI WA MLIMA KILIMANJARO KESHO

ZA KITAIFA
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kesho tarehe 21.04.2016 litazindua Kampeni Maalum ya siku 10 ya usafi wa Mlima Kilimanjaro. Uzinduzi huo Utafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Said Mecky Sadik.
Kazi hii ya kusafisha Mlima Kilimanjaro itafanywa na watumishi wa hifadhi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa utalii zaidi ya 200, wakiwemo mawakala wa utalii (tour operators), waongoza wageni (guides), wapagazi (porters) na wapishi (cooks) wanaowahudumia watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.
Usafi huu utahusisha maeneo mbalimbali ya hifadhi kama vile njia za kupandia mlimani, maeneo ya kupiga kambi, maeneo ya mabanda, na maeneo ya kupumzikia wageni (picnic sites).
Kampeni hii ni muendelezo wa utaratibu wa kawaida wa hifadhi unaofanyika kila wakati kuhakikisha maeneo ya hifadhi hasa yanayotumika na wageni yanakuwa katika viwango vya kimataifa vya utoaji huduma kwa wageni. Huu ni utaratibu wenye lengo la kuwahamasisha wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wanauweka Mlima Kilimanjaro katika hali ya usafi muda wote.
Mlima Kilimanjaro unachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 60 ambazo ni sawa na asilimia 34 kwa mwaka katika mapato ya TANAPA. Aidha, Mlima Kilimanjaro hutoa ajira zaidi ya laki tatu(300,000) kwa mwaka kwa Watanzania wanaofanya shughuli za utalii mlimani.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
20.04.2016
dg@tanzaniaparks.go.tz

Unknown

Author & Editor

Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.