Ad (728x90)

Tuna Develop/Design Blog & Website & Android Application ......0717331293

Tuesday, 18 October 2016

Filled Under:

KWA WAMILIKI WA MAGARI SOMA HII;

ZA KITAIFA
UFAHAMU: KWA WENYE MAGARI;

Matairi ya gari muda wake rasmi wa matumizi ni miaka minne ( 4 ) tu toka yatengenezwe (Sio toka uyafunge kwenye gari yako).

Ikishapita miaka minne toka tairi litengenezwe linaweza kupasuka wakati wowote. Jinsi ya kutambua tairi lilitengenezwa lini tafuta alama kwenye tairi iliyoandikwa kwa mfumo huu (*2603*) kuna kuwa na alama ya nyota mwanzo na mwisho wa hizo namba nne.

Namba mbili za kwanza zinaonyesha tairi lilitengenezwa wiki ya ngapi katika wiki 52 za mwaka na namba mbili za mwisho zinaonyesha mwaka tairi lilipo tengenezwa. Kwa mfano *2603* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 2003 au *2699* inamaanisha tairi lilitengenezwa wiki ya 26 ya mwaka 1999.

KAGUA MATAIRI YAKO USITUMIE TAIRI LILILO PITA ZAIDI YA MIAKA MINNE KWANI LINAWEZA PASUKA WAKATI WOWOTE.

Pia kila tairi limeandikwa uwezo wa spidi yake ukikimbiza zaidi ya uwezo wake itapasuka na hizo spidi zimeandikwa kwa herufi Kama ifuatavyo

CODE. SPIDI;
F========80
G ========90
J ========100
K ========110
L ========120
M ========130
N ========140
P ========150
Q ========160
R ========170
S ========180
T ========190
H ========200

Huandikwa hivi
280/R/70/13/560/S
Hapo herufi S inawakilisha spidi,180.

Unknown

Author & Editor

Naitwa Prince Emanuel, ni mtangazaji na muandaji wa vipindi kupitia Morning Star Radio na Morning Star Televesion Tanzania.

0 comments:

Post a Comment

 

Copyright © UNCLE PRINCE ™ is a registered trademark.
Designed by Templateism. Hosted on Blogger Platform.