Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Aprili, 2016
amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara.
Taarifa
iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa kati
ya Makatibu tawala hao 10 ni wapya, 2 wamebadilishiwa vituo vya kazi na 13 wamebakisha
katika vituo vyao vya sasa.
Makatibu
Tawala wapya walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
- Arusha - Richard Kwitega
- Geita - Selestine Muhochi Gesimb
- Kagera - Armatus C. Msol
- Kilimanjaro - Eng. Aisha Amour
- Pwani - Zuberi Mhina Samatab
- Shinyanga - Albert Gabriel Msovela
- Singida - Dr. Angelina Mageni Lutambi
- Simiyu - Jumanne Abdallah Sagini
- Tabora - Dkt. Thea Medard Ntara
- Tanga - Eng. Zena Said
Makatibu
Tawala waliobadilishwa vituo vya kazi ni kama ifuatavyo;
- Kigoma - Charles Amos Pallangyo (Kutoka Mkoa wa Geita)
- Morogoro - Dkt. John S. Ndunguru (Kutoka Mkoa wa Kigoma)
Makatibu
Tawala waliobakishwa katika vituo vyao vya sasa vya kazi ni kama ifuatavyo;
- Dar es salaam - Theresia Louis Mbando
- Dodoma - Rehema Hussein Madenge
- Iringa - Wamoja Ayubu Dickolagwa
- Katavi - CP Paul Chagonja
- Lindi - Ramadhan Habibu Kaswa
- Mara - Benedict Richard Ole Kuyan
- Manyara - Eliakimu Chacha Maswi
- Mbeya- Mariam Amri Mjunguja
- Mtwara - Alfred Cosmas Luanda
- Mwanza - CP. Clodwing Mathew Mtweve
- Njombe - Jackson Lesika Saitabau
- Rukwa - Symthies Emmanuel Pangisa
- Ruvuma - Hassan Mpali Bendeyeko
Makatibu Tawala wa
Mikoa 10 ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza, wataapishwa siku ya Jumatano
tarehe 27 Aprili, 2016 saa tatu asubuhi Ikulu Jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment