Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za
rambirambi Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kufuatia kifo
cha Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mama Lucy Kibaki aliyefariki dunia leo tarehe
26 Aprili, 2016.
Mama
Lucy Kibaki ambaye ni Mke wa Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki
amefariki dunia Jijini London nchini Uingereza, ambako alikuwa akipatiwa matibabu.
Katika
salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kifo hicho na kuongeza kuwa
Kenya imempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi
yake.
“Kupitia
kwako Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta napenda kumpa pole
nyingi Rais Mstaafu wa Kenya Mheshimiwa Mwai Kibaki, Familia yake, Ndugu, Jamaa
na Marafiki wote walioguswa na msiba huu mkubwa”
Amesema Rais Magufuli.
Dkt.
John Pombe Magufuli pia amemuombea marehemu Lucy Kibaki apumzishwe mahali pema
peponi, Amina.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
26
Aprili, 2016
0 comments:
Post a Comment